Dr Wilbroad Slaa kurudi nchini baada ya kukaa nje na kutoa waraka mzito kwa wanasiasa.

Month: March 2017

Dr Wilbroad Slaa kurudi nchini baada ya kukaa nje na kutoa waraka mzito kwa wanasiasa.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye kwa sasa anaishi nje ya nchi, Willbrod Slaa amesema anajitathmini kwa kile kilichomfanya aondoke hapa nchini na familia yake kama hakipo aweze kurejea nyumbani. Dkt. Slaa aliamua kuweka pembeni masuala ya siasa baada ya kutofautiana na chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea wa Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa. Amesema kuwa kwa sasa amemaliza masomo yake na baada ya kutafakari na kujitathmini atarejea nyumbani muda wowote. “Ni kweli nimemaliza masomo yangu, bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na familia yangu, baada ya hapo

Continue Reading

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn anatarajiwa kuwasili nchini kesho

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn anatarajiwa kuwasili nchini kesho, Machi 31 kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Hayo yalisemwa jana  na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Masharika, Dkt. Suzan Kolimba alipokuwa Akizungumza na waandishi wa habari. Alisema kuwa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn imetokana na mkutano kati yake na Rais Dkt. Magufuli uliofanyika baada ya mkutano wa kawaida wa 28 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika hivi karibuni huko nchini Ethiopia. Alisema

Continue Reading

Serengeti Boys yafanya kufuru kaitaba

TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Burundi jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na fainali za vijana Afrika Mei mwaka huu nchini Gabon. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mtanzania, mwenye beji ya FIFA, Deonisya Rukyaa, wenyeji walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza 2-0. Mabao hayo yalifungwa na kiungo Muhsin Makame na beki wa kushoto, Nickson Kibabage aliyepanda kusaidia mashambulizi. Makame alifunga dakika ya 19 akimalizia pasi ya Israel Mwenda kutoka upande wa kulia, wakati Kibabage alifunga dakika ya 38

Continue Reading

Clouds Kumsimamisha kazi mfanyakazi wake kwa kuandika habari za Makonda

Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima. Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa

Continue Reading

Wananchi wilayani Mbulu Mkoani Manyara watakiwa kujiunga-PPF

Wananchi wilayani mbulu mkoani manyara wametakiwa kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii PPF kwa mafao ya uzeeni na afya . Akizungumza na redio habari njema mkuu wa wilaya ya mbulu bwana CHELESTINO MOFUGA   Amesema kila mwananchi ajiunge na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF ambaoumefika kwenye wilaya ya mbulu . Aidha mkuu wa wilaya ya mbulu ametaja faida za kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ikiwa ni pamoja na kupata mkopo wa biashara . Amesema aliyejiunga na mfuko huo ataendelea kulipia na atakapo fikisha umri wa kustaafu au kushindwa kufanya kazi atapata mafao yake ya uzeeni sawa

Continue Reading

Halmashauri-Mbulu imetangaza Matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Mitaa Mitatu

Halmashauri ya mji wa Mbulu imetangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa mitaa mitatu uliofanyika hivi karibuni kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada wa viongozi hao kujihuzulu. Akizungumza na kituo hiki kaimu mkurungenzi wa halmashauri ya mji huo Bwana. Philmon Qamara amesema uchaguzi huo umelazimika kufanyika kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo viongozi hao kujihuzulu na wengine muda wao kuisha. Aidha Philmon amezitaja vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo katika halmashauri hiyo kuwa ni chama cha mapinduzi CCM ,chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na chama ACT wazelendo huku chama cha demekrasia imejinyakulia viti viwili na CCM kiti kimoja wakati ACT wazalendo hawakuambulia

Continue Reading

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, yamuachia huru Mbunge wa Kilombero-Chadema

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, imemuachia huru mbunge wa Kilombero kupitia chama cha demockrasia na maendeleo (Chadema) Peter Lijualikali. Lijualikali amekutwa hana hatia katika kesi hiyo ambayo alihukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kosa la kufanya vurugu wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015. Hata hivyo mawakili wake walikata rufaa na leo mahakama imemuona hana hatia katika madai hayo.

Continue Reading

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Moshi laazimia jambo

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro wameazimia kwa pamoja  kupitiwa upya kwa mchakato wa kuwepo kwa jiji la Moshi ambalo litahusisha baadhi ya vijiji wilayani humo. Wakizungumza katika kikao cha Baraza hilo, baadhi ya madiwani wamesema hawajashirikishwa  pamoja na wanavijiji ambao wanatakiwa maeneo yao yajumuishwe kwenye uanzishwaji wa jiji la Moshi. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael Kilawila ametoa ushauri kwa wataalamu wa halmashauri hiyo juu ya mchakato wa uanzishwaji wa jiji la Moshi. Hata hivyo Afisa Ardhi wa Wilaya ya Moshi, Cecilia Mwing’uri amesema vikao vyote vimefanyika kwa kuzishirika Halmashauri zote na

Continue Reading

Maafisa uhamiaji-Uganda wamevamia makao ya kampuni moja ya ujenzi ya China

Maafisa wa uhamiaji nchini Uganda wamevamia makao ya kampuni moja ya ujenzi ya China, na kuwakamata raia 28 wa Uchina kwa madai kuwa wanaishi na kufanya kazi nchini humo kinyume na sheria. Baadhi ya raia hao wa China walijifungia ndani ya viumba vyao, kwa kuhofia kukamatwa. Karibu watu 16 walikamywa katika kambiayao kuu iliyo kijiji cha Kyebando, mashariki mwa Uganda, huku wengine 22 wakikamatwa kwenye timbo moja la mawe. Kampuni hiyo ya China Railway, ilikuwa imeshinda zabuni ya kujenga barabara ya karibu kilomita 100 eneo hilo. Maafisa hao wa uhamiaji walikuwa wameandamana na wenzao kutoka kwa halmashauri ya barabara ya

Continue Reading

Kenya yawasailisha Bajeti yake ya 2017-2018.

Waziri wa fedha Henry Rotich anakwenda bungeni na Bajeti ya Shilingi za Kenya Trilioni 2.6, ikiwa ndio bajeti kubwa zaidi kushuhudia nchini humo. Hii ndio mara ya kwanza kwa bajeti nchini Kenya kuwasilishwa kwa wabunge mwezi Machi. Kenya na mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini yamekuwa yakiwasilisha bajeti zao kwa pamoja mwezi Juni utaratibu ambao Kenya itarejesha mwaka 2018. Hata hivyo, hali imekuwa tofauti nchini Kenya kwa sababu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu. Wabunge wengi nchini humo huenda wasiwe bungeni mwezi Aprili kuandaa bajeti hiyo kwa sababu

Continue Reading