KAMATI za Kudumu za Bunge zimeanza  shughuli zake mjini Dodoma hadi Aprili 2, mwaka huu kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Saba wa Bunge Aprili 4.

Serikali wiki ijayo itawasilisha kwa wabunge wote mapendekezo ya serikali kuhusu mpango na kiwango cha ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Bunge kamati hizo pamoja na kukutana na watendaji wa serikali katika shughuli zake pia zitatembelea maeneo mbalimbali nchini na kukagua miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Mkutano wa Saba wa Bunge unatarajiwa kuanza Aprili 4, mwaka huu ukiwa ni mkutano kwa ajili ya kuchambua, kujadili na kupitisha bajeti za wizara mbalimbali tayari kwa utekelezaji wa shughuli za serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Aidha, hoja mbalimbali zitatolewa na wabunge kuhusu tathmini ya utekelezaji wa bajeti iliyopita ili kuboresha bajeti ijayo hasa katika maeneo ya miradi ya maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *