Rais John Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuendelea kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao

Ameyasema hayo wakati  akiwahutubia wananchi katika sherehe za kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiyo mwenye uamuzi na kuwataka kuacha kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii..

Mkuu huyo wa nchi amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo badala ya kupoteza muda kufuatilia udaku kwenye mitandao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *