Halmashauri-Mbulu imetangaza Matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Mitaa Mitatu

Halmashauri ya mji wa Mbulu imetangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa mitaa mitatu uliofanyika hivi karibuni kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada wa viongozi hao kujihuzulu.

Akizungumza na kituo hiki kaimu mkurungenzi wa halmashauri ya mji huo Bwana. Philmon Qamara amesema uchaguzi huo umelazimika kufanyika kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo viongozi hao kujihuzulu na wengine muda wao kuisha.

Aidha Philmon amezitaja vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo katika halmashauri hiyo kuwa ni chama cha mapinduzi CCM ,chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na chama ACT wazelendo huku chama cha demekrasia imejinyakulia viti viwili na CCM kiti kimoja wakati ACT wazalendo hawakuambulia hata nafasi moja.

Wenyeviti walio chaguliwa kaika mitaa hizo ni kama ifuatavyo mtaa wa ujenzi ni George Alphonce wa chadema ,mtaa wa mishiqo ni Joseph Emaay ingi wa CCM na mtaa wa Manuwas ni Massay Tluway wa Chadema

Amehitimisha kwakusema kuwa uchanguzi ulikuwa wa haki na amani hivyo kila mgombea alikubaliana na matokeo hayo ya uchaguzi na hivyo hakukuwa na vitendo vya uvunjifu wa amani.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *