Kenya yawasailisha Bajeti yake ya 2017-2018.

Waziri wa fedha Henry Rotich anakwenda bungeni na Bajeti ya Shilingi za Kenya Trilioni 2.6, ikiwa ndio bajeti kubwa zaidi kushuhudia nchini humo.

Hii ndio mara ya kwanza kwa bajeti nchini Kenya kuwasilishwa kwa wabunge mwezi Machi.

Kenya na mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini yamekuwa yakiwasilisha bajeti zao kwa pamoja mwezi Juni utaratibu ambao Kenya itarejesha mwaka 2018.

Hata hivyo, hali imekuwa tofauti nchini Kenya kwa sababu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Wabunge wengi nchini humo huenda wasiwe bungeni mwezi Aprili kuandaa bajeti hiyo kwa sababu za kisiasa, na ikiwa bajeti haingewasilishwa mapema, basi ingeathirika.

Wizara ya fedha nchini Kenya, inasema licha ya makadirio ya bajeti hii kuwasilishwa mapema, yataanza kutekelezwa mwezi wa kifedha wa Juni.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *