Wananchi wilayani Mbulu Mkoani Manyara watakiwa kujiunga-PPF
Wananchi wilayani mbulu mkoani manyara wametakiwa kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii PPF kwa mafao ya uzeeni na afya .
Akizungumza na redio habari njema mkuu wa wilaya ya mbulu bwana CHELESTINO MOFUGA Amesema kila mwananchi ajiunge na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF ambaoumefika kwenye wilaya ya mbulu .
Aidha mkuu wa wilaya ya mbulu ametaja faida za kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ikiwa ni pamoja na kupata mkopo wa biashara .
Amesema aliyejiunga na mfuko huo ataendelea kulipia na atakapo fikisha umri wa kustaafu au kushindwa kufanya kazi atapata mafao yake ya uzeeni sawa na watumishi wengine ambao wako kwenye taasisi mbalimbali na serikali.
Bwana mofuga amewaomba wananchi watumie nafasi hiyo kujiunga mapema kwani kadiri wilaya inavyokuwa na wanachama wengi ndivyo mafao yatakavyoharakishwa katika kuwahudumia hasa vikundi vya akina mama na vijana.