Spika wa Bunge la Afrika Kusini ateta na Wapinzani

Day: April 4, 2017

Spika wa Bunge la Afrika Kusini ateta na Wapinzani

Spika wa Bunge nchini Afrika Kusini Baleka Mbete, amesema atafikiria na kufanya uamuzi kuhusu ombi la vyama vya upinzani nchini humo kutaka kuwasilisha mswada wa kukosa imani na rais Jacob Zuma. Upinzani unasema huu ndio wakati wa kumwondoa Zuma madarakani baada ya kumfukuza kazi Waziri wa Fedha Pravin Gordhan wiki iliyopita, hatua iliyoshutumiwa vikali na hata wabunge na viongozi wa chama tawala cha ANC. Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa upinzani nchini humo kuwasilisha mswada kama huu bungeni kujaribu kumwondoa Zuma madarakani kwa madai ya ufisadi lakini hawakufanikiwa kwa sababu ya wabunge wengi wa chama tawala. Upinzani kwa sasa unaona

Continue Reading

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya yatoa kauli

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imesema ndio yenye mamlaka ya kujumuisha na kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu nchini humo. Kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati baada ya muungano wa upinzani NASA mwishoni mwa wiki kutangaza kuwa itakuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo. Chebukati amewataka wanasiasa wa upinzani kuiamini Tume hiyo na kuwahikikishia kuwa mawakala wao watapata fursa ya kuthathmini matokeo yote yatakayotolewa baada ya zoezi la kupiga kura tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu. Kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga amesema, upinzani umeweka mikakati ya kuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo na kuyatangaza na kusisitiza

Continue Reading

Watu 10 wafariki dunia nchini Urusi

Watu 10 wamethibitishwa kupoteza maisha baada ya kutokea kwa shambulizi katika kituo cha kupanda treni cha chini ya ardhi cha mjini St. Petersburg, nchini Urusi. Taarifa zinasema shambulizi hilo lilitokea katika kituo maarufu cha Sennaya Ploshchad, na waliothirika ni wale waliokuwa ndani ya gari ya treni hiyo Idadi ya watu waliojeruhiwa haijafahamika lakini abiria wengi wameonekana wakilia maumivu  huku juhudi za kuwaokoa zikiendelea. Picha katika mitandao ya kijamii zinaonesha namna gari moshi hilo lilivyoharibika kwa ndani na milango kurushwa mbali. Hadi sasa haijafahamika waliohusika na shambulizi hili na Vituo vingine vya magari moshi katika mji huo vimefungwa kutokana na shambulizi

Continue Reading

MKUU wa Wilaya ya Hanang’ atoa onyo

MKUU wa wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara, Bi Sara Msafiri amepiga marufuku kufanya shughuli za kibiashara za mazao nje ya soko la Kimataifa la ENDAGAW. Mkuu wa wilaya hiyo ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa Bodi ya soko hilo uliofanyika katika Mji wa Katesh na kusema kuwa uchunguzi wa muda mrefu umebaini kuwa idadi kubwa ya wafanyabiashara wamekuwa wakiwadhulumu wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei ya chini kwa lengo la kukwepa ushuru wa serikali kwa kuyafuata mazao kwa wakulima. Awali katika taarifa ya soko hilo iliyosomwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hanang, na Kaimu Afisa Kilimo,

Continue Reading

Wanaume na wanawake wametakiwa kushirikiana katika vya vikoba

Wanaume na wanawake wametakiwa kushirikiana katika vikundi vya vikoba ili kujiimarisha kiuchumi . Kauli hiyo imetolewa na wananchi katika kata ya BASHNET walipokuwa wakipozungumza baada ya kutembelewa na idara ya jinsia na maendeleo jimbo katoliki la mbulu pamoja na mwakilishi wa baraza la maaskofu katoliki Ujerumani. Mtoa Elimu katika Vikundi vy kukopa na kuweka katika kata hiyo Anjela Pius amewaomba wanawake kusimama imara katika kusimamia miradi yao bila ya kushindwa ili kueleka Tanzania ya viwanda. Naye mratibu wa idara ya jinsia na maendeleo jimbo katoliki la mbulu BI: ANSILA TEMBO alipowatembelea wanafunzi wa shule ya mssingi Long amewaomba kuwa mfano

Continue Reading

SUMATRA yatoa maelekezo

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri majini na nchi na kavu (SUMATRA) Gilliard Ngewe amesema huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo nchini zitaendelea kama kawaida hapo kesho. Hatua hiyo imekuja baada ya wamiliki wa  vyombo vya usafiri nchini kuzungumza na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano,  Profesa Makame Mbarawa. Makubaliano hayo yalifikiwa mapema leo baada ya wamiliki wa mabasi (TABOA), wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UWADAR) pamoja na wamiliki wamalori(Tatoa) kuzungumza na Profesa Mbarawa na kukubaliana kubadili kanuni na kuzitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Walikubaliana kuzifanyia marekebisho kanuni hizo ndani ya siku 14 na zipelekwe kwa wadau, pia zitenganishe

Continue Reading

Wananchi Wilayani Mbulu wametakiwa kushirikiana na viongozi wao

Wananchi wametakiwa kushirikiana na viongozi wao katika juhudi za kuleta maendeleo. Ameyasema hayo Diwani wa kata ya Sanu wilayani Mbulu Africanus Mmao na kusema kuwa wananchi wamesahau kujishughilisha na mambo yatakayoleta maendeleo yao na jamii kwa ujumla isipokuwa wameanza kuwa mashabiki wa siasa. Akizungumzai ujenzi wa daraja la Hantee amesema mpaka sasa daraja hilo ujenzi umetumia umetumia shilingi bilioni tisa na kilichobi nguzo na sakafu ili liweze kupitika . Katika hatua nyingine amewapongeza wananchi wa kata ya sanu kwa kujitoa katika shughuli za ujenzi wa daraja la hilo kwa kuchangia fedha za ujenzi na kuwaomba wale ambao bado hawajachangia kumaliza

Continue Reading