Spika wa Bunge la Afrika Kusini ateta na Wapinzani

Spika wa Bunge nchini Afrika Kusini Baleka Mbete, amesema atafikiria na kufanya uamuzi kuhusu ombi la vyama vya upinzani nchini humo kutaka kuwasilisha mswada wa kukosa imani na rais Jacob Zuma.

Upinzani unasema huu ndio wakati wa kumwondoa Zuma madarakani baada ya kumfukuza kazi Waziri wa Fedha Pravin Gordhan wiki iliyopita, hatua iliyoshutumiwa vikali na hata wabunge na viongozi wa chama tawala cha ANC.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa upinzani nchini humo kuwasilisha mswada kama huu bungeni kujaribu kumwondoa Zuma madarakani kwa madai ya ufisadi lakini hawakufanikiwa kwa sababu ya wabunge wengi wa chama tawala.

Upinzani kwa sasa unaona kuwa, kutokana na uugwaji mkono wa baadhi ya wabunge wa ANC huenda mswada huo ukaungwa mkono na wabunge wengi.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *