Tume ya Uchaguzi nchini Kenya yatoa kauli

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imesema ndio yenye mamlaka ya kujumuisha na kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati baada ya muungano wa upinzani NASA mwishoni mwa wiki kutangaza kuwa itakuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo.

Chebukati amewataka wanasiasa wa upinzani kuiamini Tume hiyo na kuwahikikishia kuwa mawakala wao watapata fursa ya kuthathmini matokeo yote yatakayotolewa baada ya zoezi la kupiga kura tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga amesema, upinzani umeweka mikakati ya kuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo na kuyatangaza na kusisitiza kuwa hakuna atakayewazuia kufanya hivyo.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *