Wananchi Wilayani Mbulu wametakiwa kushirikiana na viongozi wao

Wananchi wametakiwa kushirikiana na viongozi wao katika juhudi za kuleta maendeleo.

Ameyasema hayo Diwani wa kata ya Sanu wilayani Mbulu Africanus Mmao na kusema kuwa wananchi wamesahau kujishughilisha na mambo yatakayoleta maendeleo yao na jamii kwa ujumla isipokuwa wameanza kuwa mashabiki wa siasa.

Akizungumzai ujenzi wa daraja la Hantee amesema mpaka sasa daraja hilo ujenzi umetumia umetumia shilingi bilioni tisa na kilichobi nguzo na sakafu ili liweze kupitika .

Katika hatua nyingine amewapongeza wananchi wa kata ya sanu kwa kujitoa katika shughuli za ujenzi wa daraja la hilo kwa kuchangia fedha za ujenzi na kuwaomba wale ambao bado hawajachangia kumaliza michango yao ili ujenzi ukamilike.

Amesema ujenzi wa daraja hilo utakapokamilika utapunguza adha kwa akina wamama wajawazito ,wagonjwa ,wanafunzi na jamii kwa ujumla pindi wanapohitaji kwenda kupata huduma ya afya katika hospitali ya wilaya.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *