Watu 10 wafariki dunia nchini Urusi
Watu 10 wamethibitishwa kupoteza maisha baada ya kutokea kwa shambulizi katika kituo cha kupanda treni cha chini ya ardhi cha mjini St. Petersburg, nchini Urusi.
Taarifa zinasema shambulizi hilo lilitokea katika kituo maarufu cha Sennaya Ploshchad, na waliothirika ni wale waliokuwa ndani ya gari ya treni hiyo
Idadi ya watu waliojeruhiwa haijafahamika lakini abiria wengi wameonekana wakilia maumivuĀ huku juhudi za kuwaokoa zikiendelea.
Picha katika mitandao ya kijamii zinaonesha namna gari moshi hilo lilivyoharibika kwa ndani na milango kurushwa mbali.
Hadi sasa haijafahamika waliohusika na shambulizi hili na Vituo vingine vya magari moshi katika mji huo vimefungwa kutokana na shambulizi hili.