Boko haramu latimiza miaka 3 toka utekaji wa wasichana – Nigeria

Day: April 14, 2017

Boko haramu latimiza miaka 3 toka utekaji wa wasichana – Nigeria

Miaka mitatu imepita tangu magaidi  wa Boko Haram walipowateka wasichana zaidi ya 200 kutoka shule ya Chibok Kaskazini mwa Nigeria. Serikali ya Nigeria inasema mazungumzo yanaendelea kuhakikisha kuwa wasichana wengine 195 ambao bado wanashikiliwa, wanaachiliwa huru. Wazazi wa wasichana hao kwa mwaka wa tatu sasa, wanaona kuwa serikali haijafanya juhudi za kutosha kuwaokoa wasichana wao. Haijafahamika ni wapi waliko wasichana hao, huku ikishukiwa kuwa kuna uwezekano kuwa wamejifichwa katika msitu wa Sambisa. Jeshi la Nigeria likishirikiana na mataifa mengine kama Cameroon, Niger na Chad wameunda jeshi la pamoja kuwatafuta wasichana hao.

Continue Reading

Bomu lauwa Afghanstan

Bomu kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa na Marekani na ambalo halitumii nyuklia limeangushwa kwenye milima ya Afghanistan na kuripotiwa kuwaua mamia ya wapiganaji wa kundi la Islamic State ambao wamekuwa wakijificha kwenye mahandaki. Serikali ya Afghanistan imethibitisha kudondoshwa kwa bomu hilo, ambalo pamoja na nguvu kubwa ya uharibifu inayotokana na silaha hiyo, mamlaka nchini humo zimekanusha taarifa kuwa kuna raia wa kawaida waliouawa. Bomu hilo aina ya GBU-43/B Massive Ordnance Air Blast, linafahamika kwa jina jingine kama “Mama wa mabomu yote” na limetumiwa kwa mara ya kwanza kulenga ngome za wapiganaji wa IS mashariki mwa jimbo la Nangarhar hapo jana jioni.

Continue Reading

Waendesha bodaboda na baiskeli, wapewa onyo kali

Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda na baiskeli, kuanzia leo wamepigwa marufuku kusafirisha mazao ya misitu kama vile mkaa na mbao kwa kutumia vyombo hivyo, na watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria. Imebainika kuwa kutokana na kukithiri kwa usafirishaji wa mazao hayo kwa vyombo hivyo vya usafirishaji, serikali hupoteza jumla ya fedha za maduhuli zinazokadiriwa kufikia Sh bilioni 1.1 kwa mwezi ambayo ni sawa na Sh bilioni 13 kwa mwaka. Mkakati huo wa kuwakamata watakaokiuka agizo hilo, unatekelezwa na mamlaka tatu ambazo ni Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama wa Barabarani, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra)

Continue Reading

Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Raymond Saba na Ijumaa Kuu

Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Raymond Saba amesema Ijumaa Kuu ni siku muhimu ambayo waumini wa kanisa hilo wanakumbuka fumbo la ukombozi kupitia mateso ya Yesu Kristo. Ijumaa Kuu huadhimishwa siku moja kabla ya Sikukuu ya Pasaka (kufufuka kwa Yesu),  hivyo leo Wakristo dunia wanmeadhimisha siku hiyo. Pasaka huadhimishwa ikiwa ni kumbukumbu ya mateso ya Yesu, huku viongozi wa dini wakihimiza upendo, msamaha na utu wema Amesema Pasaka inaonyesha jinsi Mungu alivyo na upendo uliomuwezesha kumtoa mwanaye mpendwa Yesu Kristo kuteswa kwa kupigwa, kubebeshwa msalaba, kuvalishwa taji la miba na kutobolewa na mkuki hadi kufa ili

Continue Reading

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu -Cherestino Mofuga anatarajiwa kuzindua Saccoss ya wanawake

Mkuu wa wilaya ya mbulu mkoani manyara Cherestino Mofuga anatarajiwa kuzindua Saccoss ya wanawake wilayani humo kwa lengo la kuendeleza kuimarisha uchumi wa wanawake. Akizungumza na kituo hiki mwenyekiti wa sacoss ya wanawake wilayani mbulu bi Sophia Silvini Amesema wanataria kuzindua sacos hiyo siku ya jumatatu ….. Aidha Sophia Silvini Amesema kuwa sacoss hiyo itawanufaisha wanawake wengi ili kujikwamua kiuchumi. Sophia Amewatawaka wanawake kujitokeza kwa wingi ili wajumuike kwa pamoja na wapate manufaa kiuchumi.

Continue Reading

Askari Polisi wanane wauawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha

Rais John Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi wanane waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani. Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu leo inasema askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi. Kutokana na tukio hilo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na

Continue Reading