Vyama vya kisiasa nchini Algeria vyaja na mpya

Day: April 20, 2017

Vyama vya kisiasa nchini Algeria vyaja na mpya

Vyama vya kisiasa nchini Algeria vimeridhia kuweka picha za wagombea wa kike kwenye mabango yake. Vyama vingi vimekua vikiweka picha za mitandio bila kuwepo na uso wa mgombea. Hata hivyo picha za wagombea wa kiume zimetawala kwenye mabango. Maafisa wa uchaguzi wameagiza vyama kuanza kuweka picha za wagombea wa kike la sivyo vitaondolewa kwenye usajili. Hatua hii imevutia hisia tofauti kutoka kwa wagombea wa kika na kiume. Mmoja wa wagombea Fatma Tirbakh wa chama cha ‘National Front For Justice’ amesema eneo anakotoka kuna mila na itikadi kali dhidi ya wanawake kujionyesha hadharani. Hata hivyo amesema anataka picha yake kuwekwa kwa

Continue Reading

Zimbabwe yasherehekea miaka 37 tangu uhuru

Zimbabwe inasherehekea miaka 37 tangu kupata uhuru chini ya rais Robart Mugabe  mwenye unmri wa miaka 93. Maadhimisho hayo yanafanyika kipindi ambacho Zimbabwe inakabiliwa na kushuka thamani kwa pesa yake hatua iliyosabisha  wizara ya elimu nchini humo kutangaza ada zilipwe kwa mfumo wa mifugo. Katibu mkuu wa wizara hiyo, Sylvia Utete-Masango alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wameandaa mfumo kwa wanafunzi kutoa mifugo kama ada kwa maeneo ya vijijini huku mijini wazazi watatakiwa kufanya  vibarua maalum mashuleni ili kufidia ada za watoto wao. Rais Mugabe ameiongoza Zimbabwe tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1980. Viongozi mbalimbali duniani wametuma salama za pongezi

Continue Reading

Wito watolewa DAWASCO

Wito umetolewa kwa watendaji wa Mamlaka ya Maji safi Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) kuongeza nguvu katika usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi kuliko kuwekeza katika Uzalishaji kama ilivyo sasa. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo wakati wa alipotembelea ofisi za Dawasco na kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo, ambapo amewataka kuongeza kasi katika usambazaji wa Maji na kuboresha miundombinu. Aidha Profesa Mkumbo ametoa rai kwa Taasisi zisizolipia huduma hiyo kusitishiwa mara moja kama ambavyo Agizo la Rais Magufuli kwa wasiolipia huduma ya Umeme kusitishiwa  huku akiwataka  waanze kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na utunzaji

Continue Reading

Sakata la Vyeti feki laibuka tena

Sakata la watumishi wa umma kugushi vyeti vya elimu limezidi kuchukua sura mpya na sasa wamefikia zaidi ya 10,000. Hatua hiyo, inatokana na uhakiki uliofanywa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ambayo imebaini waombaji kazi 39,511 kati yao, 1,951 wana vyeti vya kughushi. Kuongezeka kwa idadi hiyo, kunatokana na kauli ya Rais Dk. John Magufuli, wiki iliyopita, kwamba anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali ambao wamebainika kuwa na vyeti feki. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam, wakati akizindua mabweni mapya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alisema anafahamu idadi ya watumishi wenye vyeti feki

Continue Reading

Ajali mbaya yatokea Jijini Dar es salaam

Mtu mmoja mwanaume amefariki dunia papo hapo,huku wengine 27wakijeruhiwa baada ya Gari aina ya Eacher ambayo walikuwa wakisafiria   kugonga treni katika maeneo ya Kamata wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam majira ya saa 11 alfajiri. Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Simon Sirroamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo  nakudai kuwa chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi ambao umesababisha dereva kushindwa kulimudu gari hilo na kugonga treni wakati lilipofika kwenye njia  ya Treni. Hata hivyo Kamishna Sirro ametoa rai kwa Madereva wote kuwa makini katika kuzingatia sheria za barabarani wakati wa kupita kwenye njia  ya Reli,ili kusaidia kuepukana na ajari ambalimbali ambazo siyo za lazima.

Continue Reading

Rais John Magufuli atoa ahadi kwa madaktari

Rais John Magufuli amesema kati ya madaktari 500 walioonyesha nia ya kwenda kufanya kazi nchini Kenya watachaguliwa 258 na kuajiriwa na serikali ya Tanzania mara moja kuanzia sasa. Taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ilieleza kuwa hatua hiyo imefuatia baada ya kutetereka kwa makubalino ya serikali ya Tanzania na Kenya baada ya Mahakama nchini Kenya kutoondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira za madaktari wa Tanzania nchini humo. Rais Magufuli ameamua kuwa, madaktari hao 258 ambao walikuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na serikalini mara moja. Ummy amesema Kufuatia uamuzi huu, majina ya madaktari husika na vituo

Continue Reading

Wananchi wilayani Mbulu mkoani Manyara watolewa hofu juu ya TB

Wananchi wilayani Mbulu mkoani Manyara wametakiwa  kutokuwa na hofu yeyote baada ya wagonjwa wa kifua kikuu {TB}kuchanganywa katika wodi ya wagonjwa wengine katika hospitali ya wilaya hiyo. Hayo yamesemwa na kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Mbulu daktari Hhangali Qwaray wakati akizungumza na redio habari njema kuhusiana na baadhi ya wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo kulalamikia kuchanganywa katika wodi moja na wagonjwa wa kifua kikuu. Aidha doktari  Hhangali ameitaka jamii kuwa tabia za kupima afya zao mara kwa mara pindi waonapo dalili ya ugonjwa huu wa kifua kikuu ili kuzuia mambukizi kutoka kwa mtu mmoja ndani ya familia kwenda kwa

Continue Reading