Ajali mbaya yatokea Jijini Dar es salaam

Mtu mmoja mwanaume amefariki dunia papo hapo,huku wengine 27wakijeruhiwa baada ya Gari aina ya Eacher ambayo walikuwa wakisafiria   kugonga treni katika maeneo ya Kamata wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam majira ya saa 11 alfajiri.

Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Simon Sirroamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo  nakudai kuwa chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi ambao umesababisha dereva kushindwa kulimudu gari hilo na kugonga treni wakati lilipofika kwenye njia  ya Treni.

Hata hivyo Kamishna Sirro ametoa rai kwa Madereva wote kuwa makini katika kuzingatia sheria za barabarani wakati wa kupita kwenye njia  ya Reli,ili kusaidia kuepukana na ajari ambalimbali ambazo siyo za lazima.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *