Wananchi wilayani Mbulu mkoani Manyara watolewa hofu juu ya TB

Wananchi wilayani Mbulu mkoani Manyara wametakiwa  kutokuwa na hofu yeyote baada ya wagonjwa wa kifua kikuu {TB}kuchanganywa katika wodi ya wagonjwa wengine katika hospitali ya wilaya hiyo.

Hayo yamesemwa na kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Mbulu daktari Hhangali Qwaray wakati akizungumza na redio habari njema kuhusiana na baadhi ya wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo kulalamikia kuchanganywa katika wodi moja na wagonjwa wa kifua kikuu.

Aidha doktari  Hhangali ameitaka jamii kuwa tabia za kupima afya zao mara kwa mara pindi waonapo dalili ya ugonjwa huu wa kifua kikuu ili kuzuia mambukizi kutoka kwa mtu mmoja ndani ya familia kwenda kwa mtu mwingine.

Hata hivyo daktari amehitimisha kwakuisisitizia jamii kuzingatia  usafi wa mazingira , na kujenga nyumba ambazo zina madirisha ya kutosha  na kuzingatia usafi binafsi kama kufunga mdomo kwa kitambaa wakati wakukohoa na kupiga chafya .

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *