Watoto 20 wafariki dunia Afrika Kusini

Day: April 21, 2017

Watoto 20 wafariki dunia Afrika Kusini

akriban watoto 20 wamefariki katika ajali ya barabarani katika mkoa wa Mpumulunga nchini Afrika Kusini kaskazini mwa mji mkuu wa Pretoria. Kulingana na chombo cha habari cha Reuters, basi dogo walilokuwa wakisafiria liligonga lori na kulipuka. Russel Meiring ,ambaye ni msemaji wa shirika la matibabu ya dharura ER24 ameambia Reuters kwamba watoto 20 walikuwa ndani ya basi hilo wakati lilipogongana na lori hilo la kubeba mizigo. ”Idadi hiyo sasa inadaiwa kufika 20”, alisema. Chapisho la awali ambalo lilithibitisha watoto 13 kufariki ilionyesha eneo la ajli hilo. Panyaza Lesufi, afisa anayehusika na elimu katika mkoa wa Gauteng amesema kuwa ni ‘siku

Continue Reading

Upinzani waanzishwa upya Ivory Cost

Nchini Ivory Cost upinzani umeanzisha toka siku ya Alhamisi, Aprili 20, muungano mpya. Vyama vinne pamoja na vyama vingi vya wafanyakazi na mashirika ya kiraia yameunda muungano mpya (ESD) Georges Armand Ouégnin ndiye alituliwa kuwa kiongozi wa muungano huo. Baada ya Muungano wa CNC, na Front du refus, vyama vingine vya upinzani vimeanzisha muungano mpya toka siku Alhamisi, Aprili 20. Muungano huo unaundwa na vyama vya siasa vinne, RPP, AIRD, UNG na FPI pamoja na vyama vingi vya kiraia, ikiwa ni pamoja na Cojep, SYNAP-CI. Muungano huo mpya unaongozwa na Georges Armand Ouégnin, naibu kiongozi wa chama cha RPP, chama

Continue Reading

SADC yaanza upatanishi

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeanza upatanishi kati ya pande husika katika mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Makubaliano ya Saint-Sylvestre na utekelezaji wake ni moja ya vipengele muhimu vitakavyogubika mazungumzo hayo. Jaribio hili jipya la kutaka kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini DRC linakuja baada ya rais Joseph Kabila kumteua waziri mkuu. Ujumbe wa SADC ambako uko ziarani mjini Kinshasa tangu siku ya Jumanne, unakutana na wadau wote katika mgogoro wa Congo kwa lengo la kukusanya maoni na mapendekezo ya serikali na upinzani kwa kutatua mgogoro huo unaoendelea. Siku ya Alhamisi, Waziri wa

Continue Reading

Mwili Dkt. Elly Macha waagwa leo katika viwanja vya Bunge

Bunge la Tanzania leo limesitisha shughuli zake ili kuweza kutoa fursa kwa waheshimiwa wabunge waweze kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Chadema Dkt. Elly Macha aliyefariki dunia katika hospitali ya New Cross, nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu. Katika kile kilichoonekana kuwa  ratiba za kawaida za bunge zisiharibike Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alieleza wabunge jana kuwa bajeti ya TAMISEMI na ile ya Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora majadiliano yalitakiwa yamalizike jana hiyo hiyo ili leo shughuli za kuuga mwili wa Dkt. Macha ziweze kufanyika. Agizo hilo

Continue Reading

TAKUKURU – Rukwa,yafanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi Milioni 71

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ya TAKUKURU mkoani Rukwa,imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi Milioni 71,baada ya kufuatilia mchezo mchafu uliokuwa ukiendelea kwenye Halmashauri zote nne za mkoa huo, na kubaini malipo yaliyofanywa kwa wafanyakazi ambao tayari walikuwa wameshastaafu. Naibu Mkuu wa taasisi hiyo ya TAKUKURU mkoani Rukwa Bw Ching’oro Samamba,akitoa taarifa mjini sumbawanga amesema hayo ni matokeo ya uchunguzi ulioanza kufuatilia wafanyakazi hewa, mishahara hewa na malipo ya posho hewa kwenye halmashauri zote zilizoko mkoani humo, na kubaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa malipo ya serikali. Kwa upande wake Afisa mchunguzi wa TAKUKURU mkoani Rukwa Bw Mussa

Continue Reading

Walimu 22,993 kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara wamenufaika na mafunzo ya mtaala mpya

Walimu 22,993 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara wamenufaika na mafunzo ya mtaala mpya na uimarishaji wa ufundishaji wa stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu kwa walimu wa somo la hisabati na lugha wa darasa la tatu na la nne, yanayoendeshwa na Wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu ( ADEM ) kwa kushirikiana na Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia. Mtendaji Mkuu wa ADEM Dk.Siston Masanja amesema mafunzo hayo ya mtaala ulioboreshwa kwa sasa yanawashirikisha takribani 9,060 katika mikoa 7 ya Dodoma, Kigoma, Lindi, Mara, shinyanga, Simiyu na Tabora na kuongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ubora wa

Continue Reading

Vyanzo vya Maji vya Mto Ruaha Mkuu vyaisaidia TANESCO

Shirika la umeme Tanzania TANESCO limesema kuwa utunzaji wa vyanzo vya maji vya mto Ruaha Mkuu ambavyo vinapatikana wilaya za Wanging’ombe na Makete Mkoani Njombe unasaidia kuongeza Maji yanayohitajika katika ufuaji wa umeme kwenye mabwawa ya Mtera na Kidatu. Kaimu mkurugenzio mtendaji wa TANESCO Dr Tito  Mwinuka akiwa katika ziara ya kikosi kazi maalumu kilichoundwa Hivi karibuni na makamu wa raisi Samia Suluhu Hassani akiwa  mkoani Iringa kwaajili ya kutunza ikolojia ya mto Ruaha mkuu amesema kuwa Asilimia 41 ya umeme unaozalishwa hapa nchini unategemea maji na huwa ni bei nafuu. Mwenyekiti wa kikosi hicho  kilichopangiwa kutembelea vyanzo vya maji

Continue Reading

Madereva na abiria wa pikipiki wilayani Mbulu wameusiwa kuvaa Helmet

Wananchi wilayani mbulu mkoani manyara hususani dereva na abiria wa pikipiki wameaswa kuvaa element ili kujikinga na ajali ambazo mara nyingine hupelekea vifo vinavyosababisha upungufu wa nguvu kazi ya taifa . Hayo yamesemwa na ASP Angela John Lameck mkuu wa kituo police mbulu na amesema uvaaji wa element kwa dereva wa pikipiki na abiria ni sheria ambayo ipo na ni suala la lazima. Aidhamkuu wa kituo Angela Lameck amesema niwajibu wa abiria kuvaa element na kwamba abiria waangalie namna ambayo itawasaidia kujikinga na maradhi ambayo yanaweza kupatikana katika kofia hizo . Uvaaji wa kofia za helment kwa abiria wa pikipiki

Continue Reading

Wanasiasa wawili mashuhuri wa upinzani nchini Zimbabwe kumpindua Mugabe

Wanasiasa wawili mashuhuri wa upinzani nchini Zimbabwe wamekubaliana kuungana dhidi ya Rais Robert Mugabe. Morgan Tsvangirai na Makamu wa Rais wa zamani Joice Mujuru wamesema watashirikiana pamoja kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao. Hata hivyo haijabainika nani atakua mgombea Urais kati ya wawili hao. Bwana Mugabe wa miaka 93 amekua madarakani tangu Zimbabwe kunyakua uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1980, na amesema atatetea tena wadhifa wake. Mugabe amemepuzilia mbali muungano wowote wa upinzani na kusema hauwezi kumshinda. Mwanasiasa huyo amekua akidai kuibiwa kura na Mugabe na washirika wake. Morgan Tsvangirai aliteuliwa Waziri Mkuu katika serikali ya muungano na Rais Mugabe

Continue Reading

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA kutoa Mgombea

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umesema kuwa utamtangaza atakayeshikilia bendera yake ya urais mnamo tarehe 27 mwezi Aprili 2017. Akizungumza katika mkutano wa kumlaki gavana wa kaunti ya Bomet Isack Ruto kujiunga na muungano huo kama mmoja wa viongozi wakuu wa chama hicho, waziri wa zamani wa maswala ya kigeni ambaye pia ni seneta wa kaunti ya Bungoma Moses Wetangula amesema kuwa kiongozi huyo atatajwa katika mkutano utakaofanyika uwanja wa Uhuru Park uliopo katikati ya jiji la Nairobi. Amesema kwamba tayari viongozi hao ambao wamekuwa wakikutana kwa takriban siku tatu zilizopita wamepiga hatua ya kumchagua mmoja wao kuongoza muungano

Continue Reading