Madereva na abiria wa pikipiki wilayani Mbulu wameusiwa kuvaa Helmet

Wananchi wilayani mbulu mkoani manyara hususani dereva na abiria wa pikipiki wameaswa kuvaa element ili kujikinga na ajali ambazo mara nyingine hupelekea vifo vinavyosababisha upungufu wa nguvu kazi ya taifa .

Hayo yamesemwa na ASP Angela John Lameck mkuu wa kituo police mbulu na amesema uvaaji wa element kwa dereva wa pikipiki na abiria ni sheria ambayo ipo na ni suala la lazima.

Aidhamkuu wa kituo Angela Lameck amesema niwajibu wa abiria kuvaa element na kwamba abiria waangalie namna ambayo itawasaidia kujikinga na maradhi ambayo yanaweza kupatikana katika kofia hizo .

Uvaaji wa kofia za helment kwa abiria wa pikipiki kwa mwakan 2017 umeongezeka kwa kiasi kikubwa wilayani mbulu mkoani Manyara ikilinganishwa na mwaka 2016

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *