SADC yaanza upatanishi

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeanza upatanishi kati ya pande husika katika mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Makubaliano ya Saint-Sylvestre na utekelezaji wake ni moja ya vipengele muhimu vitakavyogubika mazungumzo hayo.

Jaribio hili jipya la kutaka kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini DRC linakuja baada ya rais Joseph Kabila kumteua waziri mkuu.

Ujumbe wa SADC ambako uko ziarani mjini Kinshasa tangu siku ya Jumanne, unakutana na wadau wote katika mgogoro wa Congo kwa lengo la kukusanya maoni na mapendekezo ya serikali na upinzani kwa kutatua mgogoro huo unaoendelea.

Siku ya Alhamisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Augustine Mahiga, anayeongoza ujumbe wa SADC amewapokea katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa, wajumbe wa chama tawala cha PPRD na washirika wake na kisha muungano wa upinzani wa Rassemblement unaoendelea kugawanyika kuhusu uteuzi wa waziri mkuu mpya.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *