TAKUKURU – Rukwa,yafanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi Milioni 71

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ya TAKUKURU mkoani Rukwa,imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi Milioni 71,baada ya kufuatilia mchezo mchafu uliokuwa ukiendelea kwenye Halmashauri zote nne za mkoa huo, na kubaini malipo yaliyofanywa kwa wafanyakazi ambao tayari walikuwa wameshastaafu.

Naibu Mkuu wa taasisi hiyo ya TAKUKURU mkoani Rukwa Bw Ching’oro Samamba,akitoa taarifa mjini sumbawanga amesema hayo ni matokeo ya uchunguzi ulioanza kufuatilia wafanyakazi hewa, mishahara hewa na malipo ya posho hewa kwenye halmashauri zote zilizoko mkoani humo, na kubaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa malipo ya serikali.

Kwa upande wake Afisa mchunguzi wa TAKUKURU mkoani Rukwa Bw Mussa Gyunah, amesema uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo ni endelevu ili kuendelea kubaini madudu yanayofanywa, na kwamba walibaini kuwa malipo mengi yaliyofanywa yalisababishwa na uzembe wa maafisa utumishi wa halmashauri hizo,na wanaendelea kuwachunguza ili sheria ichukue mkondo wake.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *