Upinzani waanzishwa upya Ivory Cost

Nchini Ivory Cost upinzani umeanzisha toka siku ya Alhamisi, Aprili 20, muungano mpya. Vyama vinne pamoja na vyama vingi vya wafanyakazi na mashirika ya kiraia yameunda muungano mpya (ESD) Georges Armand Ouégnin ndiye alituliwa kuwa kiongozi wa muungano huo.

Baada ya Muungano wa CNC, na Front du refus, vyama vingine vya upinzani vimeanzisha muungano mpya toka siku Alhamisi, Aprili 20.

Muungano huo unaundwa na vyama vya siasa vinne, RPP, AIRD, UNG na FPI pamoja na vyama vingi vya kiraia, ikiwa ni pamoja na Cojep, SYNAP-CI. Muungano huo mpya unaongozwa na Georges Armand Ouégnin, naibu kiongozi wa chama cha RPP, chama cha Laurent Dona Fologo.

Vyama vinvyunda muungano huu mpya vilisaini mkataba unaozungumzia mambo kumi na mbili ikiwa ni pamoja na maridhiano ya kitaifa,kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa, uhuru wa vyombo vya habari, sera ya fedha ya nchi au kesi ya Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude ICC .

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *