Vyanzo vya Maji vya Mto Ruaha Mkuu vyaisaidia TANESCO

Shirika la umeme Tanzania TANESCO limesema kuwa utunzaji wa vyanzo vya maji vya mto Ruaha Mkuu ambavyo vinapatikana wilaya za Wanging’ombe na Makete Mkoani Njombe unasaidia kuongeza Maji yanayohitajika katika ufuaji wa umeme kwenye mabwawa ya Mtera na Kidatu.

Kaimu mkurugenzio mtendaji wa TANESCO Dr Tito  Mwinuka akiwa katika ziara ya kikosi kazi maalumu kilichoundwa Hivi karibuni na makamu wa raisi Samia Suluhu Hassani akiwa  mkoani Iringa kwaajili ya kutunza ikolojia ya mto Ruaha mkuu amesema kuwa Asilimia 41 ya umeme unaozalishwa hapa nchini unategemea maji na huwa ni bei nafuu.

Mwenyekiti wa kikosi hicho  kilichopangiwa kutembelea vyanzo vya maji vya mto Ruaha mkuu katika mkoa wa Njombe Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe Jackson Ole Saitabau amesema lengo la kikosi hicho kuundwa ni kurudisha hali ya utiririshaji wa maji  katika mto ruaha mkuu.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *