Wanasiasa wawili mashuhuri wa upinzani nchini Zimbabwe kumpindua Mugabe

Wanasiasa wawili mashuhuri wa upinzani nchini Zimbabwe wamekubaliana kuungana dhidi ya Rais Robert Mugabe.

Morgan Tsvangirai na Makamu wa Rais wa zamani Joice Mujuru wamesema watashirikiana pamoja kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Hata hivyo haijabainika nani atakua mgombea Urais kati ya wawili hao.

Bwana Mugabe wa miaka 93 amekua madarakani tangu Zimbabwe kunyakua uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1980, na amesema atatetea tena wadhifa wake.

Mugabe amemepuzilia mbali muungano wowote wa upinzani na kusema hauwezi kumshinda.

Mwanasiasa huyo amekua akidai kuibiwa kura na Mugabe na washirika wake.

Morgan Tsvangirai aliteuliwa Waziri Mkuu katika serikali ya muungano na Rais Mugabe kati ya mwaka 2009 hadi 2013.

Joice Mujuru alikua Makamu wa Rais wa Mugabe kwa miaka 10.

Hata hivyo aliondolewa wadhifa huo mwaka wa 2014 hatua iliyompelekea kuunda chama chake cha kisiasa cha National People’s Party.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *