Picha za CCTV zinazomuonyesha Salman Abedi usiku aliofanya shambulizi katika ukumbi wa Manchester na kuwaua watu 22 zimetolewa.

Month: May 2017

Picha za CCTV zinazomuonyesha Salman Abedi usiku aliofanya shambulizi katika ukumbi wa Manchester na kuwaua watu 22 zimetolewa.

Picha za CCTV zinazomuonyesha Salman Abedi usiku aliofanya shambulizi katika ukumbi wa Manchester na kuwaua watu 22 zimetolewa. Maeneo 14 yanasakwa na wanaume 11 wamekamtwa kwa kushukiwa kuhusika katika ugaidi. Abedi alitambuliwa saa mbili baada ya shambulizi la siku ya Jumatatu. Waziri mkiu Theresa May anasema kuwa kiwango cha tisho lililopo kimepunguzwa na wanajehsi waliotumwa kuwasaidia polisi wataondolewa kuanzia siku ya Jumatatu Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionUlinzi mkali uliwekwa Wembley Mamia ya polisi waliojihami wanaendelea kulinda mamia ya tamasha kote nchini Uingereza. Mamia ya polisi walitumwa wakati mashabiki 50,000 walihudhuriw tamasha la Courteeners kwenye uwanja wa kriketi wa Old

Continue Reading

Katika michezo:Dortmund yashinda kwa mabao 2:1 dhidi ya Eintracht Frankfurt

Borussia Dortmund imeshinda kwa mara ya nne katika historia ya klabu hiyo kombe la shirikisho, DFB Pokal. Dortmund BVB iliishinda timu ya Eintracht Frankfurt kwa mabao 2-1 (1-1). Katika mechi hiyo tiketi zote za kiingilio cha uwanja wa Olimpiki wa mjini Berlin ziliuzwa. Timu hiyo imenyakua taji hilo, baada ya awali kufikia fainali mara tatu mfululizo na kushindwa mara zote. BVB ilipata bao la kuongoza kupitia mchezaji wake Ousmane Dembele katika dakika ya nane, licha ya kukosa nafasi nyingi za kufunga. Hivyo, Frankfurt ilipata nafasi kusawazisha kupitia mchezaji wake Ante Rebic katika dakika ya 29 . Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang alifunga

Continue Reading

Merkel hakuridhishwa jinsi mkutano wa G7 ulivyomalizika.

Mkutano wa viongozi wa nchi 7 zilizoendelea kiuchumi umemalizika katika kisiwa cha Sicily nchini Itallia huku hali ya kutokuelewana viongozi hao ikijitokeza. Kwa mujibu wa wanadipliomasia rais wa Marekani Donald Trump hakutaka kuukubali mkataba wa Paris wa kulinda mabadiliko ya tabia nchi. Rais Trump mwenyewe aliandika kwenye ujumbe wake wa Twitter kwamba ataamua wiki ijayo kama nchi yake itayaheshimu makubaliano hayo au la. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alionyesha kutoridhishwa kwake baada ya mkutano huo wa G7 kumalizika. Mazungumzo na Marekani yalielezwa kuwa yalikuwa magumu mno. Kulikuwepo pia na utata kuhusu masuala ya biashara huria na mgogoro wakimbizi. Katika hili

Continue Reading

Hao ndiyo waliochomwa moto wakiwa wamefumaniwa arusha. R.I.P

Continue Reading

Wafanyakazi wa Mochwari Watiwa Mbaroni kwa Kuiba Kete 32 za Dawa za Kulevya

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amefunguka kuwa wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala wameiba jumla ya kete 32 za dawa za kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa Raia wa Ghana aliyefariki dunia akiwa katika nyumba ya wageni.   Kamanda Sirro amesema wahudumu hao wanne wote wamekamatwa na kukiri kwamba  baada ya kifo cha raia huyo wa Ghana aliyefariki ndani ya ‘Red Carpet’ iliyopo Sinza Dar es Salaam walipasua mwili wa raia huyo na kutoa kete hizo kisha kuziuza, na kuongeza wametaja watu ambao wamewauzia ambao nao wamekamatwa na wapo chini ya ulinzi wa polisi “Yule Mghana

Continue Reading

Wahujumu uchumi walitaka kumhonga Rais Magufuli Bilioni 300, uchunguzi Makinikia

Ikiwa imepita siku mbili tangu Rais John Magufuli kueleza kuwa kwa sasa nchi iko katika vita ya uchumi na kwamba ana majina ya watu waliotaka kuingilia na kuharibu uchunguzi wa Kamati Maalumu aliyoiunda ili kuchunguza thamani na viwango vya madini vilivyomo kwenye mchanga wenye madini (Makinikia) katika makontena 277 yaliyozuiliwa kusafirishwa nje ya nchi, ili kupoteza ushahidi. Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole Mei 25, 2017 aliibuka na kudai kuwa kuna wahujumu uchumi walitaka kumhonga kiasi cha Bilioni 300 Rais Magufuli, ili kusitisha zoezi la uchunguzi huo, huku akihoji masilahi wanayopata watu wanaofanya biashara ya kusafirisha makinikia hayo

Continue Reading

Acacia Wataka Uchunguzi Huru Mchanga Wa Dhahabu……Watishia Kuchukua Hatua Kuhakikisha Hawapati Hasara

Kampuni ya Acacia imesema ripoti kuhusu mchanga wa dhahabu aliyopewa Rais John Magufuli Jumatano ya wiki hii imejaa upotoshaji wa hali ya juu na imependekeza kufanyika kwa uchunguzi mpya ambao ni huru ili kuweza kupata ukweli. Katika taarifa yake ya jana, Kampuni ya  Acacia, yenye makao makuu jijini London, Uingereza, imesema kwamba, imejaribu mara kadhaa kuomba nakala ya ripoti hiyo nzima pamoja na utaratibu wa kuchukua sampuli kwenye uchunguzi huo, lakini mpaka sasa haijapewa. “Kwa kuzingatia data tulizo nazo kwa zaidi ya miaka 20 ambazo tunaweza kuzitoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, hatuwezi kukubaliana na matokeo ya Tume. Data hizi

Continue Reading

Wauawa kwa kuwalinda wanawake Waislamu Marekani

Haki miliki ya pichaCBS/EVNImage captionPolisi wanasema mwanamume aliyekuwa akitukana, aliwageukia wanaume hao waliojaribu kuingilia kati Polisi katika mji wa Portland nchini Marekani, wanasema wanaume wawili waliuawa, walipojaribu kumzuia mwanamume aliyewatukana kiubaguzi, wanawake wawili, walioonekana kuwa Waislamu. Kisa hicho kilitokea kwenye treni jana. Polisi wanasema mwanamume aliyekuwa akitukana, aliwageukia wanaume hao waliojaribu kuingilia kati, na kuwadunga visu na kuwauwa. Abiria mwengine alijeruhiwa, kabla ya mshambuliaji kukamatwa. Halmashauri ya uhusiano baina ya Marekani na Waislamu, imesema Rais Trump lazima atoe kauli kulaani chuki inayozidi dhidi ya Waislamu. Imesema hali inazidi kuwa mbaya kwa sababu ya maneno ya rais na sera zak

Continue Reading

Marekani kufanya majaribio ya kudungua kombora

  Idara ya jeshi nchini Marekani kwa mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la masafa marefu lililo na uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi bara lingine. Maafisa wa Pentagon wanasema jaribio hilo litafanyika Jumatano, wiki ijayo. Kumekuwa na wasiwasi mjini Washington kuhusu uboreshaji wa miradi ya kinyuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini. Mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani anasema iwapo miradi ya Korea Kaskazini ya kutengeneza makombora haitodhibitiwa, basi taifa hilo lina uwezo wa kutengeneza kombora lenye uwezo wa kufikia Marekani Matamshi hayo yanaonyesha wasiwasi wa Marekani kuhusu mpango wa Pyongyang wa kutengeza makombora mbali

Continue Reading

Tundu Lissu Akomalia Vyeti FEKI Vya Bashite……..Aungana na Wanasheria Wenzake Kufungua Kesi Mahakamani

Wakili Tundu Lissu na wenzake wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamelikomalia vilivyo sakata maarufu la Bashite linalohusiana na tuhuma za kughushi vyeti vya kielimu linalomkabili mmoja wa wakuu wa mikoa kwa kulifikisha kortini ili lipatiwe ufumbuzi. Aidha, Lissu na wenzake hao wamedhamiria kuona kuwa kigogo huyo anayetuhumiwa kuliacha jina lake halisi la Daudi Albert Bashite kutokana na matokeo mabovu ya sekondari na kutumia jina la mtu mwingine, achukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kufungwa jela kwa kosa la kughushi ikiwa itathibitika kuwa ana hatia. Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Lissu ambaye ni Rais wa TLS, alisema

Continue Reading