Borussia Dortmund imeshinda kwa mara ya nne katika historia ya klabu hiyo kombe la shirikisho, DFB Pokal. Dortmund BVB iliishinda timu ya Eintracht Frankfurt kwa mabao 2-1 (1-1). Katika mechi hiyo tiketi zote za kiingilio cha uwanja wa Olimpiki wa mjini Berlin ziliuzwa. Timu hiyo imenyakua taji hilo, baada ya awali kufikia fainali mara tatu mfululizo na kushindwa mara zote. BVB ilipata bao la kuongoza kupitia mchezaji wake Ousmane Dembele katika dakika ya nane, licha ya kukosa nafasi nyingi za kufunga. Hivyo, Frankfurt ilipata nafasi kusawazisha kupitia mchezaji wake Ante Rebic katika dakika ya 29 . Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang alifunga bao la ushindi kwa mkwaju wa penalti baada ya mlinda mlango Lukas Hradetzky kumwangusha katika eneo la hatari mshambuliaji wa Dortmund Christian Pulišić katika dakika ya 67.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *