Mkutano wa viongozi wa nchi 7 zilizoendelea kiuchumi umemalizika katika kisiwa cha Sicily nchini Itallia huku hali ya kutokuelewana viongozi hao ikijitokeza. Kwa mujibu wa wanadipliomasia rais wa Marekani Donald Trump hakutaka kuukubali mkataba wa Paris wa kulinda mabadiliko ya tabia nchi. Rais Trump mwenyewe aliandika kwenye ujumbe wake wa Twitter kwamba ataamua wiki ijayo kama nchi yake itayaheshimu makubaliano hayo au la. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alionyesha kutoridhishwa kwake baada ya mkutano huo wa G7 kumalizika. Mazungumzo na Marekani yalielezwa kuwa yalikuwa magumu mno. Kulikuwepo pia na utata kuhusu masuala ya biashara huria na mgogoro wakimbizi. Katika hili Trump pia anadaiwa kuzuia makubaliano ya pamoja.ila viongozi hao walikubaliana kwa pamoja kwenye suala la mapambano dhidi ya ugaidi. Mkutano wa G7 wa mwaka ujao utafanyika kwenye jimbo la Charlevoix katika mkoa wa Quebec nchini Kanada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *