Sethi ataka kutibiwa na daktari wa Afrika Kusini

Month: November 2017

Sethi ataka kutibiwa na daktari wa Afrika Kusini

Dar es Salaam. Mawakili wa Harbinder Sethi wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mteja wao atibiwe na daktari maalumu kutoka Afrika Kusini. Wamesema baada ya mteja wao kufanyiwa vipimo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alielezwa hawawezi kufanya upasuaji wa puto alilonalo tumboni. Kutokana na hilo, wameomba daktari huyo wa Afrika Kusini afike nchini kwa ajili ya kumtibu Sethi au mteja wao asafirishwe kwenda Afrika Kusini kwa matibabu. Wakili Joseph Sungwa amewasilisha ombi hilo leo Ijumaa Novemba 10,2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya mwendesha mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai kueleza kesi ilipangwa kutajwa na upelelezi haujakamilika. Baada

Continue Reading

Trump: Hatutakubali biashara inayowapendelea wengine

  Image captionRais Trump amesema kuwa Marekani imejiandaa kushirikiana na mataifa ya Apec iwapo kutakuwa na bishara yenye kutopendelea upande wowote. Rais Donald Trum wa Marekani amesema kuwa Marekani haitavumilia biashara yenye upendeleo, katika hotuba yake iliojaa malalamishi katika mkutano wa mataifa ya bara Asia na yale yaliopo katika bahari ya Pacific{Apec} mjini Vietnam. Amesema kuwa Marekani imejiandaa kushirikiana na mataifa ya Apec iwapo kutakuwa na bishara yenye kutopendelea upande wowote. Bwana Trump alisema kuwa biashara huru iliathiri kazi za mamilioni wa raia wa Marekani na sasa anataka usawa kutekelezwa. Tayari ameitembelea China na Japan katika zaira yake ya mataifa

Continue Reading

Dr John Magufuli ameahidi kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Uganda.

Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli ameahidi kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Uganda. Raisi Magufuli ametoa ahadi hiyo nchini Uganda wakati akizungumza katika ziara ya kikazi aliyofanya nchini Humo. Amesema watanzania wanajua kuwa watanzania ana waganda ni ndugu hivyo ataendelea kuimarisha mahusiano na udugu ili kuimarika kiuchumi kwa nchi hizo mbili.   Raisi Magufuli amefanyaziara ya kikazi nchini uganda kwa lengo la kuweka jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka hoima nchini Uganda hadi mkoani Tanga ambalo litawezesha vijana wengi wa nchi hizo kupata Ajira. ==================

Continue Reading

Polisi: Mnunuzi wa nyumba za Lugumi alitumwa na Lugumi Mwenyewe

    Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa Dk. Louis Shika ambaye alishinda mnada wa ununuzi wa nyumba za Said Lugumi na baadae kuzua kizaa-zaa, alitumwa na Lugumi mwenyewe. Dk. Louis ambaye alifunga mnada wa nyumba hizo kwa kuahidi kulipia shilingi milioni 900, alishindwa hata kutoa robo ya kiasi hicho kwa mujibu wa masharti ya mnada hali iliyopelekea kufikishwa katika kituo cha polisi. Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linahisi kuwa alitumwa na Lugumi kutokana na mazingira ya tukio husika. “Aliwekwa na Lugumi ili kukwamisha mnada,” Mambosasa

Continue Reading

Makamu wa Rais Samia awataka polisi wa Kike kupambana na ugaid, uchochezi na wizi wa mitandao

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka polisi wanawake kupambana na vitendo vya kiuhalifu ikiwemo uchochezi, wizi wa mitandao, ujangili ugaidi na utakatishaji wa fedha haramu. Hayo ameyasema jana  Novemba 9  akifunga maadhimisho ya miaka 10 ya mtandao wa polisi wanawake yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha taaluma ya Polisi Kurasini. Makamu wa Rais alisema suala la  kuwepo kwa ulinzi  ni muhimu kwa ustawi wa nchi yetu. Alisema  kwamba  kuwepo kwa polisi wanawake kumeleta mtazamo tofauti katika jamii, watu wamekuwa wakiona polisi ni rafiki wa umma. Aliwataka polisi kufuata sheria katika matukio yote ya unyanyasaji wa kijinsia badala ya kuwaacha

Continue Reading

Dr Slaa Aajiriwa Kwenye Duka la SuperMarket Canada

  Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za majumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, imebainika. Dk. Slaa, kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2015. Kwa muda wa wiki kadhaa, ziliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa zamani wa Karatu, amemaliza masomo yake na sasa anafanya kazi katika moja ya maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini humo – Supermarket. Supermarket ya Costco anayofanya kazi Dk. Slaa akihudumu kama Mshauri wa Mauzo (Sales

Continue Reading

Janeth Masaburi Aapishwa Rasmi Kuwa Mbunge  

Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuapisha  Janeth Masaburi kuwa mbunge. Janeth aliingia bungeni akisindikizwa na wabunge wanawake wa CCM. Rais John Magufuli, Oktoba 21,2017 alimteua Janeth kushika wadhifa huo. Janeth ni mke wa marehemu Dk Didas Masaburi aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Dk Masaburi aligombea ubunge wa Ubungo na kushindwa na Saed Kubenea wa Chadema. Uteuzi wa Janeth umefanywa na Rais Magufuli kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1)(e) ya Katiba ya Tanzania inayompa mamlaka ya kuteua wabunge 10 na ulihitimisha nafasi hizo. Wateule hao ambao ni mawaziri ni; Dk

Continue Reading

Nape: CCM ikikataa kuambiwa ukweli ndiyo mwanzo wa kuanguka

    Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameonya kuwa endapo chama hicho hakitataka kuambiwa ukweli na kukosolewa, utakuwa mwanzo wa kuanguka kwake. Nape aliyewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, amesema endapo CCM itaua utamaduni wa kukosoana kupitia vikao itapoteza mwelekeo. “Hiki chama tukifika mahali tukaanza kufanyiana unafiki kwamba hatutaki kuambiana ukweli tunapokosea utakuwa ndiyo mwanzo wa kuanguka kwa CCM.” Amesema hayo juzi nyumbani kwake eneo la Kisasa mjini Dodoma katika mazungumzo maalumu na Mwananchi. Nape ambaye leo anatimiza miaka 40 ya kuzaliwa, ameeleza kusikitishwa na namna ya baadhi ya watu aliowaita “vijana wa CCM”, kupotosha

Continue Reading

Magufuli: Tanzania sio shamba la kuchungia mifugo wa taifa jirani

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuwakamata mifugo watakaoingia nchini humo kutoka taifa jirani. Akizungumza katika mkoa wa Kagera ambako ameanza ziara yake ya kikazi Magufuli amesema kwamba Tanzani sio shamba la kuchungia mifugo ya nchi jirani na kwamba ataichukulia mifugo hatua kali za kisheria mifugo yoyote. Vilevile ameitaka nchi Jirani kuchukua hatua kama hiyo iwapo mifugo ya Tanzania itaingia nchini humo kinyume na sheria “Tanzania sio shamba la kuchungia mifugo ya nchi jirani, ndio maana tumeamua kukamata mifugo na kuchukua hatua kwa mujibu wa kisheria, na hata huko kwenye nchi jirani wakishika mifugo ya

Continue Reading

habarinjemafm.org/wp-admin

Image captionShambulizi nchini Marekani baisikeli na miili ya watu ilitapakaa ardhini Meya wa mji wa New York, Bill De Blasio, amearifu kwamba watu 8 wamefariki dunia na zaidi ya 12 wamejeruhiwa na gari iliyowagonga waendesha baiskeli mjini humo. Bill amelielezea tukio hilo kuwa la ugaidi lililosababisha hofu mjini humo. Kamishna wa polisi wa jiji wa New York, James O’Neill, amemuelezea mtu aliyewtekeleza tukio hilo kuwa ni kijana wa miaka 29 aliyekuwa anaendesha gari ndogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi. Alisema gari hilo liliwagonga watembea kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na basi la shule. Kwa upande wake bwana

Continue Reading