Dr John Magufuli ameahidi kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Uganda.

Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli ameahidi kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Uganda.

Raisi Magufuli ametoa ahadi hiyo nchini Uganda wakati akizungumza katika ziara ya kikazi aliyofanya nchini Humo.

Amesema watanzania wanajua kuwa watanzania ana waganda ni ndugu hivyo ataendelea kuimarisha mahusiano na udugu ili kuimarika kiuchumi kwa nchi hizo mbili.

 

Raisi Magufuli amefanyaziara ya kikazi nchini uganda kwa lengo la kuweka jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka hoima nchini Uganda hadi mkoani Tanga ambalo litawezesha vijana wengi wa nchi hizo kupata Ajira.

==================