Askofu Isaac A. Massawe ateuliwa kuwa Askofu mkuu Jimbo kuu la Arusha

Month: December 2017

Askofu Isaac A. Massawe ateuliwa kuwa Askofu mkuu Jimbo kuu la Arusha

Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Josephat Louis Lebulu wa Jimbo kuu la Arusha, Tanzania la kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Isaac Amani Massawe wa Jimbo Katoliki Moshi, kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo Kuu la Arusha, Tanzania. Askofu mkuu mteule Isaac Amani Massawe, alizaliwa tarehe 10 Juni 1951 huko Mango, Jimbo Katoliki la Moshi. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 29 Juni 1975. Tarehe 21 Novemba 2007 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi na kuwekwa wakfu tarehe 22

Continue Reading