Polisi Dar Yatoa ONYO Kwa Waliopanga Kuandamana

Month: April 2018

Polisi Dar Yatoa ONYO Kwa Waliopanga Kuandamana

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wananchi wote kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa maandamano yanayozungumzwa hayapo na ni batili.   Akizungumza leo Jumatano Aprili 25 na shirikisho la waendesha bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, ACP Sweethbert Njwele amesema jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha kila mtu anafanya shughuli zake kama kawaida bila uvunjifu wowote wa amani.   “Niwahakikishie jeshi la polisi tumejipanga na mkoa wetu utaendelea kubaki salama hakuna maandamano yatakayofanyika hivyo kila mtu aendelee na shughuli zake kama kawaida,” amesema Njwele.   Amesema waendesha bodaboda ni

Continue Reading

Puto Alilowekewa Tumboni Kigogo IPTL Hatarini Kupasuka

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa hali ya kigogo wa IPTL, Harbinder Sethi inazidi kudhoofika na puto alilowekwa tumboni linaweza kupasuka wakati wowote.   Hayo yamedaiwa leo mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Wakili wa Sethi, Hajra Mungula ambapo amedai puto hilo linaweza kupasuka na kuhatarisha maisha yake.   Wakili Mungula aliutaka upande wa mashtaka kueleza upelelezi wa kesi hiyo umefikia katika hatua gani kwa sasa kwani Aprili 11,  ilitolewa amri ya mahakama Sethi apelekwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.   “Nashukuru Aprili 18,2018 mshtakiwa alipelekwa Muhimbili, akafanyiwa kipimo cha

Continue Reading

Mbunge Aichambua Ndege ya Emirates iliyotua Nchini

Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga amesema ndege aina ya Airbus 380, EK701 ya Shirika la Ndege ya Emirates si ya kwanza yenye ukubwa huo kutua nchini kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.   Akizungumza  leo Aprili 25 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mwaka 2018/19, Mlinga amesema ndege ya kwanza kubwa kutua nchini ni aina ya Antonov mwaka 2009 ikiwa imepakia mitambo ya kufua umeme ya Richmond.   “Iliyokuja kipindi kile (Antonov) ilikuwa na uzito tani 285 wakati hii iliyokuja jana ina tani 276. Iliyokuja kipindi kile ilikuwa na injini sita, ila hii iliyotua

Continue Reading

Maandamano huko Kiongozi,Maisaka Babati

Wakaazi wa kijiji cha Kiongozi kata ya Maisaka mjini Babati wamekataa maadhimio ya halmashauri ya kijiji katika kikao kilichofanyika tarehe 12 mwezi wa nne mwaka 2018 chini ya mwenyekiti wa kijiji hicho thomas  lohay  kuuza mlima kwa mkandarasi Rock Tronick. Wamesema kuwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha za miradi mbalimbali ya kijiji,wanahofia hata fedha zitazotokana na mlima huo hazitowasaidia hivyo hawaoni haja ya kuuzwa na kumueleza mkurugenzi kuwa watafute maeneo mengine ili nao wanufaike. Wakieleza malalamiko hayo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji Fortunatus Fwema katika mkutano mkuu wa kijiji   wameaanisha miradi mbali mbali ambayo haiendani na kiwango cha fedha zilizotumika wakitolea

Continue Reading