JIMBO KATOLIKI LA MBULU LAPATA ASKOFU MPYA

Month: May 2018

JIMBO KATOLIKI LA MBULU LAPATA ASKOFU MPYA

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Anthony Lagwen kutoka Jimbo Katoliki la Mbulu, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Mbulu, nchini Tanzania. Askofu mteule Anthony Lagwen alizaliwa tarehe 5 Julai 1967 huko Tlawi, Jimboni Mbulu. baada ya masomo yake ya msingi, alibahatika kuendelea na masomo ya sekondari katika Seminari Ndogo ya Sanu, Jimbo Katoliki la Mbulu. Akapata masomo ya falsafa kutoka Seminari kuu ya Ntungamo, iliyoko Jimbo Katoliki la Bukoba na baadaye akahamia Seminari kuu ya Kipalapala, Jimbo kuu la Tabora ili kuendelea na masomo ya kitaalimungu. Tarehe 18 Oktoba 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki

Continue Reading

Panya watano wafikishwa polisi kwa kula pesa

Mfanyibiashara mmoja kutoka nchini Uganda amewapeleka panya watano katika Kituo cha Polisi cha Kotido Central katika tukio la kushangaza lililowaacha wanakijiji wenzake midomo wazi. Peter Lojok Longolangiro aliwatuhumu ‘watuhumiwa ’ watano kwa kuharibu pesa zake alizokuwa ameweka ndani ya sanduku. Mtandao wa Watchdog Uganda, umesema Longolangiro alidai kuwa panya hao walikula fedha za kenya  KSh 10,000 sawa na shilingi 227404 za kitanzania, ambazo alifikisha mbele ya  kituo cha polisi kama ushahidi. Mfanyibiashara huyo pia alilishtaki shirika la kulinda wanyamapori la Uganda kwa kushindwa kulinda wanyama wake. Alidai kuwa panya hao waliingilia faragha yake na kuingia ndani ya kisanduku hicho alichokuwa

Continue Reading

Mambo matano aliyoyasema JPM Bandarini ikiwemo kupandisha cheo

Leo May 15, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuliamefanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es salaam na kukagua matanki ya mafuta ya kupikia. Nakusogezea MAMBO MATANO aliyoyasema JPM Bandarini ikiwemo kumpandisha cheo aliyekuwa Kaimu Kamishna TRA Bandari ya DSM Ben Usaje kuwa Kamishna kamili TRA bandarini hapo baada ya kusimamia vyema uchunguzi alioagiza ufanyike bandarini. Rais Magufuli amebaini kuwa baadhi ya makontena yaliyodaiwa kuwa na mafuta ghafi (mafuta ya kupikia) yalikuwa na mafuta masafi. Rais Magufuli amesema “Wafanyabiashara wanaotumia nafasi zao kulaghai watu, huwa mnawasikia kwenye vyombo vya habari wanasema mwaka huu mafuta yamepanda bei, nawaomba tuwe wazalendo. ‘Crude Oil’ ichajiwe bei

Continue Reading

MKONGOMANI WA YANGA ATAJA KITAKACHOWAFANYA WASHINDE DHIDI YA RAYON

Baada ya Yanga kuanza vibaya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo, amesema kuwa ni lazima washinde mechi yao ijayo dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda. Yanga ilianza hatua hiyo kwa kufungwa mabao 4-0 na USM Alger ya Algeria ambapo keshokutwa Ju­matano itacheza na Rayon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Katika michuano hiyo, Yanga imepangwa Kundi D pamoja na USM Alger ya Algeria, Rayon Sport (Rwanda) na Gor Mahia kutoka Kenya. Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Zahera alisema: “Hatukuweza kufanya vizuri kwenye mchezo wa kwanza kutokana

Continue Reading

RAYON WAICHUKULIA YANGA KAMA TIMU DHAIFU

Baada ya kuwasili nchini jana wakiwa na wachezaji wao wote muhimu kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa Rayon Sports waeleza kuwa Yanga ni timu dhaifu. Rayon wameeleza kuichukulia Yanga kama timu dhaifu kufuatia kushindwa kushinda jumla ya mechi zake saba zilizopita kwenye ligi na nje ya ligi. Rayon wamesema kuwa wanaichukulia Yanga kwa namna hivyo huku wakiamini itakuwa mechi nyepesi kwao kupata matokeo. Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kesho ukiwa ni wa pili kwenye hatua hiyo

Continue Reading

AZAM FC WAACHANA NA MSHAMBULIAJI WAO MGHANA BERNARD ARTHUR

MSHAMBULIAJI Mghana, Bernard Arthur amevunja mkataba na klabu ya Azam FC ya Dar es Saalam baada ya nusu msimu tu wa kuwa na timu hiyo ya bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake. Arthur ambaye kwa Ghana mara ya mwisho alichezea Liberty Professionals ya kwo, amevunja mkataba na timu hiyo ya Dar es Salaam kutokana na kupewa muda wa kutosha wa kucheza. Licha ya kuwa na mwanzo mzuri kwenye Ligi Kuu ya Vodacpm Tanzania Bara akianza na kufunga bao katika mechi yake ya kwanza, Mghana huyo akatofautiana na kocha mpya Mromania, Cioaba Aristica aliyeanza kumuweka benchi mchezaji

Continue Reading

RAIS MAGUFULI AOMBWA KUIKABIDHI SIMBA SC KOMBE JUMAPILI TAIFA

RAIS MAGUFULI AOMBWA KUIKABIDHI SIMBA SC KOMBE JUMAPILI TAIFA RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kwamba amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli kuwakabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, Simba SC Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam, Karia amesema kwamba wanasubiri majibu kuhusu ombi hilo. Pamoja na hayo, Rais Karia amesema kwamba siku hiyo kama Rais Magufuli atakubali mwaliko huo, ataanza kwa kukabidhiwa Kombe la ubingwa wa

Continue Reading

Mke wa Trump afanyiwa upasuaji wa figo

Mke wa Rais Donald Trump, Melania Trump amefanyiwa upasuaji wa figo katika hospitali ya Walter Reed Medical Center. Kwa mujibu wa msemaji wa Melania, Stephanie Grisham amesema upasuji huo umekuwa wenye mafaninikio makubwa na hakukuwa na matatizo yoyote yaliyojitokeza. Naye Rais Trump amethibitisha hilo kupitia mtandao wake wa Twitter huku akiwashukuru wote waliokuwa wakimuombea mkewe. Taarifa za kufanyiwa upauaji huo zilitolewa na Ikulu ya Marekani Jumatatu hii huku ikidaiwa kuwa ataendelea kubakia hospitali kwa wiki yote hii ili kuweza kupata nafuu zaidi.

Continue Reading

Kiongozi wa Kundi la Kigaidi la ADF Uganga Aliyekamatwa Tanzania Afikishwa Mahakamani

Kiongozi wa kundi la waasi la Allied democratic forces Jamil Mukulu, amefikishwa Mahakamani Kuu inayohusika na uhalifu wa kimataifa mjini Kampala, Uganda, Jumatatu miaka 3 baada ya kukamatwa nchini Tanzania. Kikao cha mahakama cha jana Jumatatu  kilikuwa cha kushauriana jinsi kesi dhidi ya Mukulu na wenzake 38 itaendeshwa. Akiwa amefungwa pingu mikononi na minyororo miguuni, Jamil Mukulu na wenzake 38 walifikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali wa kikosi cha polisi cha kupambana na ugaidi. Washukiwa hao waliendelea kufungwa pingu na minyororo hata baada ya kuwa tayari wako ndani ya mahakama hiyo. Kwa mwongozo wa Jaji Eva Luswata, kikao cha jana 

Continue Reading

Marekani yafungua rasmi ubalozi wake Jerusalem

Marekani imeufungua rasmi ubalozi wake Jerusalem huku Wapalestina zaidi ya 40 wakiuawa na wengine wakijeruhiwa kwenye mapambano na askari wa Israel katika harakati za kuipinga hatua hiyo. Hatua ya Marekani ya kuuhamishia rasmi ubalozi wake kwenye mji  wa Jerusalem kutoka Tel Aviv imetekelezwa baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Aidha, balozi wa Marekani nchini Israel, David Friedman amesema kuwa baada ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa taifa la Israel wakati muhimu kama huu ni wa kihistoria kwa sababu ya ujasiri wa mtu mmoja tu ambaye ni rais wa Marekani Donald Trump ameweza

Continue Reading