Walimu wa Moi Girls wafanyiwa uchunguzi wa DNA Kenya katika kesi ya ubakaji wa mwanafunzi

Month: June 2018

Walimu wa Moi Girls wafanyiwa uchunguzi wa DNA Kenya katika kesi ya ubakaji wa mwanafunzi

Image captionMaandamano yamefanyika mjini Nairobi siku ya Jumatatu kulalamika kuhusu tuhuma za ubakaji katika shule ya Moi Girls Nairobi Walimu pamoja na wafanyakazi wengine wakiume katika shule ya upili ya Moi Girls Nairobi wametakiwa kufanyikwa uchunguzi wa DNA wakati maafisa wa upelelezi wanajaribu kuchunguza tuhuma za kubakwa kwa mwanafunzi katika shule hiyo Ijumaa usiku. Polisi wamewaagiza walimu hao wa kiume, walinzi na jamaa wa kiume wa walimu wanaoishi ndani ya Shule hiyo au wale wanaoaminika kuwa walikuwa ndani ya shule hiyo mapema Jumamosi asubuhi. Uchunguzi huo wa DNA ni muhimu katika kubaini kesi za unyanyasaji wa kingono na hutumika kumithilisha

Continue Reading

Mbunge Chadema Airushia Tuhuma Nzito Wizara ya Fedha

Mbunge wa Momba (Chadema), David Salinde amesema Wizara ya Fedha na Mipango ndio adui namba moja wa maendeleo ya Taifa na kushauri Bunge liichukulie hatua ili kutekeleza maagizo yake. Silinde akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ya mwaka 2018/19, jana Juni 4, 2018 bungeni, alisema: “Kwa lugha nyepesi kabisa, adui namba moja ni Wizara ya Fedha na Mipango. Wizara ya fedha inashindwa kutoa fedha ambazo zipo kisheria.” Silinde amesema ukiangalia ripoti za CAG, wizara imekusanya fedha lakini haipeleki sehemu husika. “Leo watu wa korosho wanalalamika wamekusanya Sh91 bilioni, wamepelekewa Sh10 bilioni,”alisema na kuongeza; “Wana sababu moja tu, uhakiki

Continue Reading

Spika Ndugai Aionya Serikali….Atishia Kuzuia Mkutano wa Bunge Mwezi Oktoba

Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameitaka serikali kuhakikisha inatekeleza agizo lake la mwishoni mwa mwaka jana kuhusu kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya kuitangaza Dodoma kuwa makao makuu ya nchi vinginevyo atazuia kufanyika kwa mkutano ujao wa Bunge. Novemba 17, mwaka jana, Spika Ndugai aliitaka serikali kuhakikisha muswada huo unasomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano uliofuata uliofanyika kwa wiki mbili kuanzia Januari 30, lakini haikufanya hivyo. Muda mfupi kabla ya kusitisha kwa muda kikao cha Bunge jijini Dodoma jana mchana, Spika Ndugai alikumbusha kuhusu agizo lake hilo na kumuonya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,

Continue Reading

Mapacha walioungana kuzikwa kaburi moja

Marehemu mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (20) waliofariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita mjini hapa watazikwa katika kaburi moja kesho. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mapacha hao watazikwa pamoja japo kunatengenezwa majeneza mawili. Alisema kwa kuwa wakati wa uhai wao mapacha hao walishakataa kutenganishwa, uongozi wa mkoa unatengeneza majeneza mawili kwa sababu ni watu wawili, lakini watazikwa kwenye jeneza moja lenye miili miwili. Hata hivyo, misalaba itakuwa miwili kwa sababu ni watu wawili tofauti, alisema Kasesela. Alisema familia za baba na mama wa mapacha hao

Continue Reading

Polisi Shinyanga Wakamata Silaha Za Kivita,waua Majambazi Wanne Makaburini Kahama

Watu wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi eneo la makaburi  ya Kitwana kata ya Busoka tarafa ya Kahama Mjini wilayani Kahama wakati wakijaribu kuwatoroka askari waliokuwa kwenye msako mkali wa kuwatafuta majambazi wanaojihusisha na matukio ya uhalifu katika wilaya hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari katika makaburi ya Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama jana Jumatatu Juni 4,2018,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule alisema tukio hilo limetokea Juni 3,2018 majira ya saa sita na dakika 40 mchana. Amewataja waliouawa kuwa ni Minani Deo (33) mkazi wa Mabanda Burundi ambaye pia ni muagizaji

Continue Reading