Tuzo Nyingine kwa Dkt. Magufulu

Month: December 2019

Tuzo Nyingine kwa Dkt. Magufulu

Shirika lisilo la Kiserikali la Kuinua Diplomasia ya Uchumi Tanzania (TEDEF) limetambua juhudi na kuthamini kazi anazofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025 inafikiwa. TEDEF imemtunuku tuzo Rais Dkt. Magufuli  na kuwa miongoni mwa Watanzania 10 waliofanya vizuri kwa kutoa mchango wao katika kuimarisha Diplomasia ya Uchumi wa nchini. Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli na kuwakabidhi tuzo hizo watanzania wengine waliomstari wa mbele kuinua diplomasia ya uchumi nchini Desemba 5, 2019 katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es

Continue Reading

Sumaye Ang’atuka

Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye leo Desemba 4, 2019 ametangaza kuondoka CHADEMA. Akiongea leo kwenye mkutanao wake na waandishi wa Habari, Sumaye amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na figisu alizofanyiwa baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa. Ameeleza kuwa alitaka kugombea nafasi ya Uenyekiti ili kuondoa dhana iliyopo miongoni mwa watu kua nafasi ya Mwenyekiti ndani ya CHADEMA ni ya Freeman Mbowe na haiguswi. ==>>Hapo chini kuna nukuu ya mambo aliyayasema leo; “Lile tangazo lililotoka jana, ilikuwa ni kweli kutoka kwenye Ofisi yangu lakini halikutengenezwa kwa lengo lile kwa hiyo naomba mliache kama lilivyo. ¬†

Continue Reading