Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara linamshikilia Evamery Thomas

Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara linamshikilia Evamery Thomas (43) mkazi wa Mawemairo kata ya Magugu kwa kosa la kukutwa na dawa za Kulevya aina ya Mirungi akiwa kwenye gari aina ya Costa linalofanya Safari za Arusha-Babati.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea 27/04/2022 katika kizuizi cha magari Minjingu.

ACP Kuzaga amesema Mtuhumiwa alibeba Mirungi bunda kumi akiwa ameweka tumboni  na kujifanya kuwa na  Ujauzito.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *