Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Jenista Mhagama amesema

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Jenista Mhagama, amesema mishahara ya watumishi wa umma itapanda ifikapofika Julai 2022 ambapo sasa wizara imeanza kupitia taarifa za watumishi katika mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara.

Waziri Mhagama amesema ofisi yake imejipanga kupandisha mishahara ya Watumishi wa Umma kwa wakati kama alivyoelekeza Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi  duniani

Amesema ofisi yake itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha ifikapo Julai, 2022 kila mtumishi wa umma anapata mshahara mpya.

Amewataka watumishi wa umma kuwa watulivu wakati zoezi hili likiendelea kushughulikiwa na Serikali.

Waziri huyo amewataka Maafisa Utumishi wote katika taasisi za umma nchini kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo kila mwongozo utakaotolewa na ofisi yake kwa lengo la kukamilisha zoezi la upandishaji wa mishahara ya watumishi.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *