Jamii imeshauriwa kuzingatia ujenzi kwa kufuata sheria za mipango miji

Jamii imeshauriwa kuzingatia ujenzi kwa kufuata sheria za mipango miji katika maeneo mbalimbali nchini ili kuweza kupata msaada wa haraka pindi yanapotokea majanga ya moto kwenye makazi yao.

Akizungumza kwa njia ya simu na kituo hiki Afisa Habari wa Jeshi la Zima moto na Uokoaji Mkoa wa Manyara, Chande Abdalah katika maadhimisho ya wiki ya Zima Moto.

Aidha,Chande amesema wananchi wakifuata utaratibu huo itasaidia kwa Jeshi la Zima moto na Uokoaji kuwafikia kwa urahisi katika kutoa huduma pale inapohitajika.

 

Wiki ya Zima moto Kitaifa ilianza April 30, 2022 na kilele chake  kimeadhimishwa May 8,2022 yenye kauli mbiu Uchumi Imara utajengwa  kwa kuzingatia kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *