mbunge mbulu vijijini aruka sarakasi kudai barabara ya lami.

Mbunge wa Mbulu Vijijini (CCM) Flatei Massay ameruka sarakasi bungeni ikiwa ni kuonyesha msisitizo wa hoja yake kuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imekuwa ikitoa ahadi ya ujenzi wa barabara ya Mbulu hadi Haydom bila utekelezaji.

Flatei ameruka sarakasi wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka 2022/2023.

Flatei amesema licha ya kuahidiwa ujenzi wa barabara hiyo tangu katika bajeti ya mwaka jana, Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeonyesha fedha zilizotengwa mwaka jana zimepelekwa kulipa madeni.

Amesema katika kitabu cha bajeti cha mwaka huu imeonyeshwa kuwa barabara hiyo itajengwa katika kiwango cha lami lakini kwa Kilometa 25.

About RHN 87.5FM

Page with Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *