UZINDUZI WA MFUMO MPYA WA KUTUMA MAOMBI YA UMEME

 

Wananchi Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wametakiwa kutuma maombi ya umeme kwa njia ya mtandao ambayo inarahisisha upatikanji wa huduma hiyo.

Hayo yamesemwa na meneja wa TANESCO wilaya ya Mbulu Mhandisi Faustina Tuya alipokuwa akizungumza na kituoa hiki kuhusu huduma mpya ya kuomba umeme kimtandao ijulikanayo kama NIKONEKT.

Naye mteja wa kwanza kuunganishwa umeme kwa  kuomba umeme kupitia mtandao amesema kuwa huduma hiyo ni nzuri kwa kuwa haichukui muda mrefu.

Mhandisi Faustina Tuya amesema kuwa huduma hiyo inamuwezesha mteja kuomba umeme mahali popote alipo bila kufika katika ofisi za TANESCO huku akiwataka kuwatumia wakandarasi wenye leseni wanapofanya wayaring.

 

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *