Watanzania wahimizwa kupata chanjo ya uviko19

Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani ametoa wito kwa wananchi kwenda kupata chanjo ya uviko 19 ili kujikinga na maradhi ya virusi vya korona.

Ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na wananchi katika uwanja waKaitaba Mkoani Kagera,ambapo amesisitiza pia wananchi kujiandaa kwa ajili ya kuhesabiwa.

Raisi Samia yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya siku tatu ambapo ameendelea kukagua miradi ya maendeleo huku akitoa wito kwa viongozi kuchapa kazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *