Rais Samia afanya uteuzi wa mkuu wa majeshi ya ulinzi

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Jacob John Mkunda kufanya kazi kwa kuanza pale alipoishia  Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ambaye amestaafu rasmi wadhifha huo leo, baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka saba.

Rais Samia ametoa agizo hilo wakati Jenerali Jacob John Mkunda akila kiapo katika wadhifa huo pamoja na viongozi wengine walioteuliwa Ikulu Jijini Dare es Salaam.

Aidha,Rais Samia amempongeza mstaafu Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kwa utendaji wake wa kazi katika kulitumia taifa na kwamba serikali itampangia majukumu mengine ili kuendelea kulitumikia taifa.

Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo amestaafu rasmi wadhifha huo leo, baada ya kuhudumu wadhifa huo kwa kipindi cha miaka saba.

About RHN 87.5FM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *