Rais Samia afanya uteuzi wa mkuu wa majeshi ya ulinzi

Rais Samia afanya uteuzi wa mkuu wa majeshi ya ulinzi

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Jacob John Mkunda kufanya kazi kwa kuanza pale alipoishia  Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ambaye amestaafu rasmi wadhifha huo leo, baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka saba. Rais Samia ametoa agizo hilo wakati Jenerali Jacob John Mkunda akila kiapo katika wadhifa huo pamoja na viongozi wengine walioteuliwa Ikulu Jijini Dare es Salaam. Aidha,Rais Samia amempongeza mstaafu Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kwa utendaji wake wa kazi katika kulitumia taifa na kwamba serikali itampangia majukumu mengine ili kuendelea kulitumikia taifa. Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo

Continue Reading

Watanzania wahimizwa kupata chanjo ya uviko19

Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani ametoa wito kwa wananchi kwenda kupata chanjo ya uviko 19 ili kujikinga na maradhi ya virusi vya korona. Ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na wananchi katika uwanja waKaitaba Mkoani Kagera,ambapo amesisitiza pia wananchi kujiandaa kwa ajili ya kuhesabiwa. Raisi Samia yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya siku tatu ambapo ameendelea kukagua miradi ya maendeleo huku akitoa wito kwa viongozi kuchapa kazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Continue Reading

Utunzaji wa mazingiza Tarafa ya Daudi Mbulu Mkoani Manyara

Jamii imeshauriwa kupanda miti kwa wingi ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwani shughuli za binadamu ndizo zinazochangia pa kubwa uharibifu wa mazingira. Kufahamu zaidi kuhusu hilo mwanahabari wetu Benigna France amefanya mahojiano na mchungaji Methew Msaganda  wa kanisa la Adventist wa Sabato Daudi Mbulu Mkoani Manyara ambapo anaanza kueleza namna ambavyo mungu amempa mwanadamu jukumu la kuyatunza mazingira. Ni sauti yake mchungaji Methew Msaganda wa kanisa la Adventist wa Sabato Daudi  akihitimisha mazungumzo na mwanahabari wetu Benigna France kuhusu Umuhimu wa kupanda miti ili kutunza mazingira.

Continue Reading

UZINDUZI WA MFUMO MPYA WA KUTUMA MAOMBI YA UMEME

  Wananchi Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wametakiwa kutuma maombi ya umeme kwa njia ya mtandao ambayo inarahisisha upatikanji wa huduma hiyo. Hayo yamesemwa na meneja wa TANESCO wilaya ya Mbulu Mhandisi Faustina Tuya alipokuwa akizungumza na kituoa hiki kuhusu huduma mpya ya kuomba umeme kimtandao ijulikanayo kama NIKONEKT. Naye mteja wa kwanza kuunganishwa umeme kwa  kuomba umeme kupitia mtandao amesema kuwa huduma hiyo ni nzuri kwa kuwa haichukui muda mrefu. Mhandisi Faustina Tuya amesema kuwa huduma hiyo inamuwezesha mteja kuomba umeme mahali popote alipo bila kufika katika ofisi za TANESCO huku akiwataka kuwatumia wakandarasi wenye leseni wanapofanya wayaring.  

Continue Reading

mbunge mbulu vijijini aruka sarakasi kudai barabara ya lami.

Mbunge wa Mbulu Vijijini (CCM) Flatei Massay ameruka sarakasi bungeni ikiwa ni kuonyesha msisitizo wa hoja yake kuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imekuwa ikitoa ahadi ya ujenzi wa barabara ya Mbulu hadi Haydom bila utekelezaji. Flatei ameruka sarakasi wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka 2022/2023. Flatei amesema licha ya kuahidiwa ujenzi wa barabara hiyo tangu katika bajeti ya mwaka jana, Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeonyesha fedha zilizotengwa mwaka jana zimepelekwa kulipa madeni. Amesema katika kitabu cha bajeti cha mwaka huu imeonyeshwa kuwa barabara hiyo itajengwa katika kiwango cha lami

Continue Reading

utunzaji wa ziwa tlawi

Karibu msikilizaji katika kipindi cha Mazingira Nyumba yetu, leo tunajadili kuhusu utunzaji wa ziwa Tlawi lilipo Mbulu Mkoani Manyara. Kufahamu mengi zaidi unagana nami mtangazaji wako  Benigna France.

Continue Reading

Jamii imeshauriwa kuzingatia ujenzi kwa kufuata sheria za mipango miji

Jamii imeshauriwa kuzingatia ujenzi kwa kufuata sheria za mipango miji katika maeneo mbalimbali nchini ili kuweza kupata msaada wa haraka pindi yanapotokea majanga ya moto kwenye makazi yao. Akizungumza kwa njia ya simu na kituo hiki Afisa Habari wa Jeshi la Zima moto na Uokoaji Mkoa wa Manyara, Chande Abdalah katika maadhimisho ya wiki ya Zima Moto. Aidha,Chande amesema wananchi wakifuata utaratibu huo itasaidia kwa Jeshi la Zima moto na Uokoaji kuwafikia kwa urahisi katika kutoa huduma pale inapohitajika.   Wiki ya Zima moto Kitaifa ilianza April 30, 2022 na kilele chake  kimeadhimishwa May 8,2022 yenye kauli mbiu Uchumi Imara

Continue Reading

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Jenista Mhagama amesema

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Jenista Mhagama, amesema mishahara ya watumishi wa umma itapanda ifikapofika Julai 2022 ambapo sasa wizara imeanza kupitia taarifa za watumishi katika mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara. Waziri Mhagama amesema ofisi yake imejipanga kupandisha mishahara ya Watumishi wa Umma kwa wakati kama alivyoelekeza Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi  duniani Amesema ofisi yake itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha ifikapo Julai, 2022 kila mtumishi wa umma anapata mshahara mpya. Amewataka watumishi wa umma kuwa watulivu wakati zoezi hili likiendelea kushughulikiwa

Continue Reading

Jamii imeshauriwa kuwa na utaratibu wa kupanda miti katika mazingira

Jamii imeshauriwa kuwa na utaratibu wa kupanda miti katika mazingira tunayoishi ili kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. Ushauri huo umetolewa na Afisa Misitu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Michael Gwandu wakati akiongea na kituo hiki na  amesema ofisi hiyo ina mikakati mingi ya kuhakikisha misitu inatunzwa pamoja na mpango wa kuhaikisha kila kaya iwe na eneo la miti iliyopandwa hadi kufikia 2025 Aidha,Gwandu amesema kila mtu anapaswa kutekeleza sheria ya utunzaji wa misitu kutokana na ukubwa wa faida zake katika jamii.

Continue Reading

Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara linamshikilia Evamery Thomas

Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara linamshikilia Evamery Thomas (43) mkazi wa Mawemairo kata ya Magugu kwa kosa la kukutwa na dawa za Kulevya aina ya Mirungi akiwa kwenye gari aina ya Costa linalofanya Safari za Arusha-Babati. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea 27/04/2022 katika kizuizi cha magari Minjingu. ACP Kuzaga amesema Mtuhumiwa alibeba Mirungi bunda kumi akiwa ameweka tumboni  na kujifanya kuwa na  Ujauzito.

Continue Reading